Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amekabidhi mahitaji ukiwemo mchele tani mbili kwa wazee 3,000 wanaoishi mazingira magumu katika kata 36 na mitaa 181 Jijini Mbeya.
Dkt. Tulia amekabidhi mahitaji hayo, Desemba 20, 2024 na kuweka bayana lengo ni kuhakikisha wazee wanaungana na watanzania kusherehekea sikukuu ya Krismas.
Amesema lengo lingine la msaada huo ni kuwapa tabasamu wazee na watu wenye ulemavu kuhakikisha wanaungana na watanzania wengine kusherekea sikukuu hiyo.
"Watanzania tujenge utamaduni wa kuwashika mkono wazee ili watabasamu kwa kutambua furaha uongeza siku za kuishi,"amesema.
Dkt. Tulia amefafanua kuwa awamu hii walengwa ni wale wenye hali duni ambao hawajiwezi na kubainisha katika awamu nyingine watayagusa makundi mengi.
"Naomba msijikie vibaya ambao hampo kwenye orodha kwani tulitoa maelekezo kwa viongozi wenu kwa walengwa tulio wahitaji ambao wamepewa mchele kilo 2 na kiasi cha Sh. 5,000"ameongeza.
Kapwile Kapwile ambaye ni mnufaika wa msaada huo, amemshukuru Dkt. Tulia na kueleza kwamba ni Mbunge wa kwanza Jimbo la Mbeya mjini kukumbuka kundi la watu wenye uhitaji.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments