ILALA YAKADIRIA KUKUSANYA BIL 130 MWAKA 2025

 

Jitihada za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha miaka mitatu ya Utawala wake, zimewezesha Serikali kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato ambapo inatarajia kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 130, kupitia mapato ya Wafanyabiashara katika Halmashauri ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

 

Akielezea kuhusiana na makadirio ya mapato hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kuwa, mafanikio ya ukusanyaji mapato hayo yatatokana na jitihada za wafanyabiashara hao ambao wamepata matumaini ya kufanyabiashara zaidi baada ya Serikali ya Rais Samia, kuruhusu Soko la Kariakoo kufanya biashara kwa saa 24.

 

Amesema, hapo awali makusanyo yalikuwa chini kidogo kutokana na mazingira ya ufanyajikazi ambapo, wafanyabiashara walifanya shughuli zao nyakati za mchana pekee na hivyo kuweka makadirio ya Halmashauri kuingiza Shilingi Bilioni 81 kwa mwaka 2022/2023, ambapo pamoja na mazingira hayo, waliweza kuvuka malengo ya makusanyo kwa asilimia 100.

 

Makusanya ya mapato kwa mwaka 2023/2024 yalikadiriwa kufikia Shilingi Bilioni 89, ambapo pia Halmashauri ilivuka malengo kwa kukusanya Shilingi Bilioni 120 na hivyo kufanya Serikali kutarajia kuongezeka kwa mapato kwa Shilingi Bilioni 130 kwa mwaka 2025, endapo mazingira ya wafanyabiashara yataendelea kuboreshwa sambamba na usalama katika maeneo ya kufanyia biashara.

 

"Ilala ndio Wilaya pekee yenye wafanyabiashara wengi kuliko Wilaya zote nchini, Halmashauri ya Ilala inatakiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 130, na hii pesa itapatikana endapo watu watafanyabiashara na sio kukaa,” amesisitiza.

 

“Makusanyo haya ni zaidi ya Halmashauri zote nchini, na pesa hizi zitapatikana endapo mazingira ya biashara na usalama vitakuwepo, na  hivi vyote vitawezekana endapo kila mtu atapiga goti, kumuombea Rais Samia maisha marefu na Afya,” amesisiza Mpogolo.

 

Amemshukuru Rais Samia, kwa kuwezesha mazingira kwa Wanyabiashara wa Kariakoo na Machinga na kuruhusu biashara kufanyika kwa saa 24 sambamba na kuweka taa za kutosha ambazo zitaendelea kuwekwa, hii imesaidia mtu kuweza kufanya mauzo mara mbili na kuingiza kipato, ikilinganishwa na hapo awali ambapo mfanyabiashara alifanya mauzo kwa saa 12 tu.

 

“Jinsi mfanyabiashara anapokuwa na mazingira mazuri ya biashara zake na akafanya kwa bidii ndivyo mapato ya Serikali yatakavyoongezeka, hivyo kuruhusu biashara mpaka usiku itasaidia pia kupunguza msongamano katika maeneo hayo  kwakuwa, wengine wataamua kuepuka msongamano, wataenda kufanya manunuzi usiku,” amesema DC Mpogolo.

 

Zaidi ya asilimia 92 ya wananchi Ilala ni wafanyabiashara na hii ni kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabiashara na kukusanya kodi nyingi kuliko Wilaya yoyote hapa nchini.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments