SERIKALI YAONDOA CHANGAMOTO YA USAFIRI VITUO VYA AFYA LUDEWA

 

Serikali ya awamu ya Sita, chini ya Uongozi Bora wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwajali Wananchi wake kwa kuboresha mazingira katika Sekta ya Afya, ambapo imekabidhi Vyombo vya usafiri ikiwemo pikipiki pamoja na magari ya huduma za dharura (Ambulance), kwenye vituo vyote vya kutoa huduma za afya Wilayani Ludewa Mkoani Njombe.

 

Wananchi hao wa Mkoa huo wameendelea kunufaika na matunda ya jitihada za Serikali ya Rais Samia, ambapo amefanya mambo makubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wake.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa gari mpya ya huduma za dharura (Ambulance) kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Ludewa iliyotolewa na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dkt. Isack Chussi amesema, Wilaya hiyo ni moja ya Wilaya yenye vituo vingi vya afya pamoja na Hospitali zinazofikia 81, ambapo mpaka sasa vituo vyote vya afya vimepata gari ya wagonjwa na sasa hospitali yao imeongezewa gari ili kuboresha ufanisi kwenye usafiri.

 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Castory Kibasa amesema, licha ya magari waliyopata lakini Serikali imetoa pikipiki ambapo naye Mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga, ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi ili kusukuma maendeleo.

 

"Nimejitahidi sana kutafuta magari tena sio ya Halmashauri peke yake hata Taasisi zingine, ukienda Polisi,TFS,na TANESCO tunahangaikia gari la kubeba nguzo kwa hiyo ndugu zangu niwahakikishie hamkufanya makosa kunituma niwawakilishe,"

amesema Kamonga.

 

Nao baadhi ya wananchi wa Ludewa akiwemo Athman Haule pamoja na Merry Mlelwa wameshukuru kuongezewa usafiri huo utakaorahisisha kusafirisha wagojwa inapotokea dharura.

 

#KhomeinTvUpdates

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments