Mama mzazi wa watoto mapacha waliokuwa wameungana Hadija Shabani Omar ametoa shukurani zake kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kugharamia matibabu ya watoto wake kwa mwaka mzima.
Watoto hao ambao ni Hassan na Hussein wenye umri wa miaka mitatu walikuwa wameungana kifua, tumbo na nyonga tayari wameshafanyiwa upasuaji na kutenganishwa.
Mwanamama huyo anamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kumgharamia katika kipindi cha mwaka mmoja walipokuwa nchini wakipatiwa matibabu na kusimamia safari yao ya kwenda Hospital King Abdulaziz Medical City iliyopo Saudi Arabia.
"Namuomba Rais Samia aje kuwaona watoto hawa pale tutakaporejea nyumbani."
Upasuaji huo uliofanikiwa umewaacha watoto hao kila mmoja akiwa na mguu mmoja mmoja.
Mama wa watoto hao pia ameishukuru Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwa naye kipindi chote cha Matibabu tangu wanatoka Tabora hadi sasa.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments