Tamasha la Msangamkuu Beach Fstival linatarajia kuanza Disemba 27 hadi Disemba 31,2024 ikiwa ni msimu wa Nne kufanyika, likiwa na lengo la kutangaza vivutio vya Utalii pamoja na Uwekezaji kwenye Mkoa wa Mtwara .
Akizungumza leo disemba 17 ,2024 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, amesema kuwa Tamasha hilo linatumika kutangaza sehemu ambazo ni vivutio vya Utalii hasa katika fukwe za bahari, na kwamba kwa msimu huu wa Nne kumekuwepo na maboresho ukilinganisha na misimu ya nyuma, ambapo kutakuwa na Wanyama kama Simba, Fisi na Pundamilia.
“Tamasha hili tunalitumia kutangaza fursa za Utalii, kwa Watanzania wote hata familia wapate nafasi ya kukaa pamoja na kubarizi maeneo ya fukwe. Pia tutaonesha ngoma za asili kutakuwa na michezo pamoja burudani kama vile beach soccer (Soka la Ufukweni), pia kutakuwa na wasanii ambao watakuja kutumbuiza”. Amesema Kanali Sawala na kuongeza
“Kutakuwa kuna nyama choma kwa mfano, nyama choma hii itakuwa ni Wanyama wa kawaida lakini kumbuka hata wale ambao kibali kimepatikana cha Wanyama kutoka kwenye mapori yetu. Uje uonje nyama choma ya Swala na Wanyama wengine ambao watapatikanika kulingana na vibali vilivyopo.”
Amesema kitu kingine cha tofauti msimu huu ni kwamba watu watapata fursa ya kuwashuhudia Wanyama kama Simba, Fisi na Pundamilia kutokana na maandalizi yaliyofanyika msimu huu.
Kwa Upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Msangamkuu Beach Festival, Emmanuel Mwambe amesema kuwa tamasha hilo limetoa fursa kwa watu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na Mikoa jirani Kujumuika pamoja katika Fukwe hizo wakiwa na Famlia zao.
#KhomeinTvUpdates
✍️Ramla Masali-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments