MIILII YA WANAFUNZI 6 WALIOGONGWA NA GARI CHUNYA YAAGWA

 

Miili ya wanafunzi Sita waligongwa na basi la kampuni ya Safina Coach, imeagwa Jumapili Julai 27 mwaka huu katika viwanja vya Shule ya Msingi Chalagwa iliyopo Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. 

 

Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa chama na serikali wameshiriki wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbarak Batenga.

 


Wadau wengine ni pamoja na Mfanyabiashara wa Madini Wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya, Geofrey Mwankenja ambaye ametoa ubani wa Sh 5.5 milioni kwa familia  za wanafunzi waliopoteza maisha baada ya kugongwa na basi hilo.

 

Ibada hiyo pia imehudhuriwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Lupa, Masache Kasaka.

 


Ajali hiyo ilitokea Julai 26 majira ya saa 11.30 alfajiri wakati wakikimbia mchaka mchaka katika kijiji cha Itumba Kata ya Chalangwa Wilayani humo na kusababisha vifo vya wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Chalangwa  Sita na tisa kujeruhiwa.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments