POLISI, MGAMBO WASAKWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA RAIA IRINGA

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linawasaka Askari namba F.4987 Sajenti Rogers wa Kituo cha Polisi Ipogolo na Askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) aitwaye Thomas Mkembela kwa tuhuma za kumuua Nashon Kiyeyeu (23) Mkazi wa Nyamhanga Manispaa ya Iringa.

 

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Allan Bukumbi amesema kuwa, Chanzo cha mauaji hayo, inadaiwa Disemba 14, 2024 Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye hakumtaja kwa jina kuwa anamtuhumu Nashon Kiyeyeu kuwa amemwibia simu yake.

 

Askari namba F.4987 Sajenti Rogers wa Kituo cha Polisi Ipogolo, ambaye anatuhumiwa kufanya mauaji. 

Aidha kamanda Bukumbi amesema kuwa sajenti Rogers kwa kushirikiana na  Mgambo huyo walimkamata mtuhumiwa na inadaiwa walimpiga na walipoona amepoteza fahamu walimpeleka Hospitali moja binafsi na baadaye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na ilivyobainika kuwa ameshafariki dunia hivyo walitoweka na kukimbilia kusikojulikana.

 

Hata hivyo Polisi Mkoa wa Iringa inaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao pamoja na kusambaza taarifa Mikoa mbalimbali.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Iringa

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments