SERIKALI YA AWAMU YA SITA YATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI

 

SERIKALI ya Awamu ya Sita, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatambua mchango wa Sekta binafsi katika Uwekezaji na imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini.

 

Serikali hii iliyoleta mabadiliko katika Sekta ya Uwekezaji katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia, imesisitiza kuwa Sekta binafsi inajukumu muhimu katika maendeleo ya Tanzania, ikichangia katika kuongeza ajira, uvumbuzi, Pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

 

Ili sekta binafsi iweze kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi, Serikali inaendelea kuboresha Mazingira ya biashara nchini na imefuta na kupunguza baadhi ya ada na tozo kero takriban 379.

 

Awali Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani alidhihirisha hadharani kwamba “Uchumi wa Taifa letu utajengwa na Sekta binafsi ambapo kati ya watanzania Milioni 61.7, walioajiriwa na Serikali ni Milioni moja tu na Milioni 60.7 waliobaki ni kutoka Sekta binafsi,” Dkt. Ashatu Kijaji alimnukuu Rais Samia, Agosti 11, 2023 wakati akifanya kikao na Wafanyabiashara Mkoani Morogoro, alipokuwa Waziri wa Viwanda na Biashara kwa kipindi hicho.

 

Katika kulitekeleza hilo, Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira bora ya biashara na kuvutia uwekezaji nchini hususani katika kukuza mazingira thabiti yanayowezesha Watanzania kuonyesha vipaji vyao, kama ilivyothibitishwa na 'Impact Business Breakfast' (IBB), yenye jukumu muhimu katika maendeleo ya Taifa.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah kwa niaba ya Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, wakati wa Hafla ya Tuzo za Biashara za Impact za 2024, amebainisha kuwa, Serikali itaendelea kuunga mkono matukio kama IBB, kwani ni muhimu kwa kupata maarifa mapya yanayohitajika kuendeleza uchumi wa nchi.

 

“Chini ya Rais Dkt. Samia, Serikali inatambua umuhimu wa ubunifu kutoka kwa Wataalamu wetu na itaendelea kuunga mkono wabunifu, IBB ni jukwaa linalowaleta pamoja makundi matatu muhimu ya Wataalamu kwa lengo la kuwahamasisha na kuwawezesha kubadilisha uzoefu, kundi A (usimamizi wa juu), B (usimamizi wa kati), na Kundi C (vijana wataalamu), wakiongoza katika sekta mbalimbali.” amesema.

 

Jukwaa hilo linaandaa mikutano ya mara mbili kwa mwezi inayowapa wafanyabiashara maarifa muhimu kuhusu kanuni za biashara zilizo thibitishwa ili kuimarisha uwezo wao wa usimamizi wa biashara na utendaji kazi.

 

Mbinu ya kipekee ya IBB inaleta wataalamu kutoka sekta mbalimbali pamoja kubadilishana uzoefu, maarifa, na mbinu bora za maendeleo ya biashara ambapo mada ya Tuzo za Biashara za Impact 2024 ni Jukumu la Sekta Binafsi katika Kufikia Ajenda ya Maendeleo ya Kitaifa ya Tanzania.

 

Serikali ya Rais Samia imeondoa vikwazo mbalimbali vilivyoonekana kukwamisha ukuaji wa Sekta binafsi, ambao ndio mhimili katika kukuza uchumi wa Taifa.

 

Pia imeimarisha mazingira ya biashara kwa kufanya marekebisho katika Sera na Sheria za biashara ili kuondoa vikwazo vinavyowakabili wafanyabiashara na wawekezaji. 

 

Hatua hizi zimejumuisha kuboresha taratibu za usajili wa biashara, kupunguza urasimu, na kuongeza uwazi, kutoa fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali kama vile kilimo, nishati, miundombinu, utalii, viwanda na kuanzisha maeneo maalum ya uwekezaji.

 

Serikali imewekeza katika miundombinu ya usafirishaji, nishati, maji na mawasiliano ambayo ni muhimu kwa shughuli za uwekezaji na biashara, hatua hii inalenga kuimarisha mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.

 

Huku ikizidi kuwa muhimu kama sehemu muhimu ya ukuaji wa uchumi na utaratibu wa ajira, Sekta binafsi hutoa bidhaa na huduma, huzalisha mapato ya kodi kwa ajili ya kufadhili miundombinu muhimu ya kijamii, na kiuchumi na pia hubuni masuluhisho mapya na ya kibunifu, kisaidia kutatua changamoto za maendeleo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments