Katika kutekeleza azma ya kujali Wananchi wake, Serikali ya awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeonyesha kujali na kuthamini maisha ya Watanzania kwa kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea Disemba, 2023 kwa wakazi wa Kata za Katesh, Jorodom na Gendabi Wilayani Hanang, Mkoani Manyara.
Nyumba hizo za kisasa zilizojengwa katika eneo la Gidagamowd katika Kitongoji cha Waret, Mkoani Manyara, zimekebidhiwa kwa wananchi Disemba 20, 2024, na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu amesema kuwa, Mradi huu ni ushahidi wa dhamira ya Serikali kusaidia wananchi kurejea katika maisha yao ya kawaida baada ya kupoteza wapendwa wao, mali, na makazi yao ili waweze kuendelea na maisha yao kama ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupatwa na maafa hayo.
Tunawapongeza wanufaika wote na tunatoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana kufanikisha mradi huu, Kwa pamoja tunaijenga Tanzania imara na yenye matumaini.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments