SERIKALI YA RAIS SAMIA YASISITIZA ABIRIA KUPEWA TIKETI ZA KIELEKRONIKI

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewaasa abiria kuhakikisha wanapatiwa tiketi za kielektroni zenye taarifa zao sahihi pindi wanaposafiri na mabasi ya masafa marefu, kwani Mfumo huo umeunganishwa na LATRA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na hivyo kurahisisha ufuatiliaji wa Bima kwa ajili ya fidia wawapo safarini.

 

Agizo hilo limetolewa kufuatia Serikali ya awamu ya Sita, kufanya jitihada katika kuhakikisha usalama wa Watanzania na haki zao, unazingatiwa wakati wa safari zao.

 


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habiba Suluo, amebainisha hayo baada ya ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na LATRA kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, katika Kituo cha Mabasi Magufuli Jijini Dar es Salaam Disemba 21, 2024.

 

Lengo likiwa ni kuangalia hali ya usafiri na kuimarisha usalama wa vyombo vya usafiri kipindi cha Sikukuu za mwisho wa mwaka, pamoja na kuangazia utekelezaji wa masharti ya leseni ikiwemo matumizi sahihi ya Kitufe cha Utambuzi wa Dereva (i- Button), matumizi sahihi ya Tiketi mtandao pamoja na Jeshi la Polisi kupima kiwango cha ulevi kwa madereva wa mabasi ya masafa marefu.

 


“Ni jukumu letu kuhakikisha mabasi yapo na abiria wanasafiri kwa nauli tuliyopanga, na tumebaini kuwa hali ni nzuri na abiria wote wamesafiri usiku na asubuhi ya leo tumekagua na kuona tiketi zimetolewa lakini kuna tatizo dogo kwa abiria wanaoshuka njiani, mfano abiria wanaopanda magari yanayokwenda Musoma na kushuka Morogoro hawapewi tiketi na hii ni hatari kwa usalama wao,”amesema CPA Suluo.

 

Amewasihi abiria kutumia Mfumo wa PIS unaopatikana kwa anwani ya https://pis.latra.go.tz/ ili kufahamu mwendokasi wa basi na endapo watabaini mwendo hatarishi wa dereva, wapige simu bila malipo kwa LATRA kupitia namba 0800110019 au 0800110020 saa 24 siku zote.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments