SERIKALI YAENDELEA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME

 

Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Nishati yaendelea  kusimamia utekelezaji wa miradi ili kuhakikisha uwepo wa umeme wa uhakika nchini. 

 

Hayo yamedhihirishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu alipotembelea miradi mbalimbali ya uzalishaji na usafirishaji umeme inayoendelea kwa lengo la kufahamu utekelezaji wa miradi hiyo na maendeleo yake Disemba 21, 2024 jijini Dar es Salaam.

 

Pamoja na kukagua miradi hiyo ya umeme inayoendelea, Dkt. Kazungu ametembelea vituo mbalimbali vya umeme kwa lengo la kuhakikisha kuwa vinafanya kazi ipasavyo na hivyo kuendelea kutoa uhakika wa uwepo wa umeme wa kutosha nchini.

 

Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Kazungu amekagua mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Ubungo I, II na III, na amekagua maendeleo ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Kimara – Ubungo – Mabibo hadi Ilala pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mabibo.

 

Vilevile ametembelea kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I, II na Kinyerezi I Extension pamoja na kukagua maendeleo ya ufungaji wa Transfoma ya ukubwa wa 175MVA katika kituo hicho.

 

Dkt. Kazungu pia ametembelea vituo vya kupoza umeme vya Gongo la Mboto na Mbagala na kukagua maendeleo ya ufungaji wa Transfoma zenye uwezo wa 120 MVA kila moja katika vituo hivyo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments