Jitihada za utekelezaji wa usimikaji wa mashine namba nne ya kufua umeme, katika Mradi wa umeme wa Bwawa la Julius Nyerere umefanikiwa kwa kiwango cha juu kwa kufikia asilimia 100 ambapo kwa sasa mashine hiyo ipo kwenye majaribio huku mashine namba 3 ikiwa kwenye asilimia zaidi ya 87 za usimikwaji.
Mradi huo wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere, ni mafanikio chanya ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Ras Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha Taifa linazalisha umeme wa kutosha na kuondokana na tatizo la uhaba wa Nishati hiyo muhimu kwa jamii.
Katika kuhakikisha utekelezaji huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora zaidi, Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umetembelea mradi huo wa kufua umeme, ili kujionea kasi ya maendeleo ya ujenzi na kuweka mkazo kwa Wasimamizi kuhakikisha usimikaji mashine nne zilizobakia unafanyika ipasavyo ili umeme utakapozalishwa uingizwe kwenye Gridi ya Taifa kwa mafanikio yatakayoleta tija inayotarajiwa kwa Watumiaji wa umeme.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Gissima Nyamo-Hanga amesema kuwa, kwa sasa jumla ya mashine tano zimekamilika kwa asilimia 100 yaani mashine namba 9, 8, 7, 6 na 5 na tayari zimeanza uzalishaji wa umeme.
Amesema, kukamilika kwa mashine namba nne ya kufua umeme kwa asilimia 100, zinadhihirisha kuwa kiwango cha utendaji kazi ni kizuri.
"Tumetembelea mradi huu kujionea shughuli zinazoendelea na kuweka msisitizo wa usimamizi bora kwa maeneo ambayo bado hayajakamilika ambapo utekelezaji kwa ujumla umefikia asilimia 99.55 huku shughuli za uzalishaji wa umeme zikiwa zimeanza.” amesema.
Tayari wastani wa megawati 1175 zinazozalishwa kutoka mashine tano za mradi huu zimeingizwa kwenye grid ya Taifa na zimeanza kutumika.
Gissima ameishukuru , Serikali ya Rais Dkt. Samia, pamoja na Wizara ya Nishati na viongozi wake wote kwa namna ambavyo mara zote imeunga mkono kwa kutoa fedha na ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa mradi mpaka kufikia hatua iliyopo sasa pamoja na miradi mingine mingi inayoendelea nchini.
”Ninawaahidi Watanzania wenzangu kuwa, sisi kama viongozi wa TANESCO tutahakikisha tunasimamia mradi huu kwa dhati na umadhubuti mkubwa ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kuleta tija ya kiuchumi na kijamii katika taifa letu la Tanzania” amehitimisha Gissima.
Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere tayari umeanza kuleta matumaini makubwa ya Kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini ikiwa ni kati ya juhudi kubwa za Rais Samia, katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments