Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Buruan imeendelea kuvinadi vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya mkoa huo.
Wiki hii Balozi Dkt. Batilda amempokea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Denis Londo ofisini kwake na miongoni mwa taarifa alizompatia ni kuhusu sehemu ya vivutio hivyo.
Londo, amefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa akiwa katika ziara ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye Kituo cha Huduma za Pamoja cha Mpakani (OSBP) kilichopo Horohoro wilayani Mkinga, kinachozihudumia nchi za Tanzania na Kenya.
Balozi Dkt. Batilda akautaja utalii wa miti ya asili na baridi, unaopatikana kwenye Hifadhi ya Asili ya Magamba, iliyopo ukanda wa milima ya Usambara Magharibi, umbali wa takribani kilomita 25 kutoka Lushoto mjini.
Amesema, kwenye msitu huo, kuna handaki lenye urefu wa ndani wa mita 50 lililochimbwa na kutumika wakati wa utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utalii wa Kiswahili cha mwambao, mavazi kama khanga na vyakula vikiwemo chapati za kurasa, ndizi za mkono wa tembo, yai la jicho la mke mwenza lenye nyama ya kusagwa ndani yake, mbaazi za kukata na chai ya kukaanga, hifadhi za Mkomazi na Saadani.
Naye Londo, amepongeza jitihada za ukuzaji utalii mkoani Tanga zinazosimamiwa na Balozi Dk Batilda, na kushauri kuwa hatua za kuchukua ni kwa LGAs kuyamiliki maeneo ya fukwe hasa yasiyokuwa na umiliki, ili yatumike katika shughuli za utalii wa ufukweni.
Londo amesema Tanga ni miongoni mwa mikoa ya kimkakati kwa uchumi na masuala mengine ya kitaifa, hivyo fursa zote zikiwemo za utalii, zinapaswa kubainishwa na kutumika ipasavyo.
Kwa mujibu wa Londo, yapo baadhi ya maeneo ya fukwe nchini yaliyomilikishwa kwa watu binafsi, na hati zake kutolewa zikiwa na hadhi ya makazi, hali ambayo ni kinyume na makusudio ya matumizi sahihi ya fukwe za bahari.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments