Uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kusaini mkataba wa kuanza ujenzi wa soko la kimkakati katika eneo la Kagunga Halmashauri ya Wilaya Kigoma, utasaidia kusogeza huduma kwa wananchi, lakini pia ni sehemu ya kudumisha ujirani mwema kutokana na kuwa soko hilo lipo katika mpaka wa Tanzania na nchi jirani ya Burundi ambalo litagharimu Shilingi Bilioni 5.6.
Tukio hili la utiajii saini mkataba huo, limefanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, ambapo ujenzi wa soko hilo la Kimataifa katika kata ya Kagunga, litawezesha wafanyabiashara wa ndani na nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kufanya biashara na kukuza uchumi.
Utiaji Saini Mkataba wa Ujenzi wa Soko hilo, umeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Bw. Joseph Nyambwe na kusisitiza mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi wa soko hilo GOPA CONTRACTORS kuzingatia makubaliano ya mkataba ili mradi ukamilike kwa wakati.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kigoma Bw. Linus Sikainda amesema, hadi kukamilika ujenzi wa soko hilo utakuwa umegharimu Shilingi Bilioni 5.6, ambapo awamu ya kwanza tayari Serikali imetoa Bilioni 2, Ili kuanza utekelezaji wa mradi wa soko hilo na kwamba, mradi huo utakuwa chachu ya kuongeza pato la Halmashauri na kuwa sehemu ya kitega Uchumi kikubwa kwa Halmashauri.
Kwa upande wake, Mkandarasi aliyepewa Tenda ya Ujenzi wa soko hilo, Godfrey John Mwogera kutoka kampuni ya GOPA CONTRACTORS, ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita, kwa kuwaamini wakandarasi wazawa na kwamba ni hatua muhimu kutekeleza miradi kwa ubora na kuhakikisha inaleta chachu ya maendeleo ya jamii na Taifa.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments