Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa katika Sekta ya Uwekezaji, ambapo inatarajia kusafirisha Tani 10 za asali kwenda nchini China kwa majaribio, zikiwa na thamani ya zaidi Milioni 100 za Kitanzania.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika Disemba 25,2024 Jijini Dar es Salaam Dkt. Jafo amesema, usafirishaji wa asali hiyo ni mafanikio makubwa na ni fursa ya kufungua milango kibiashara nje ya nchi.
Aidha, Dkt.Jafo ameshuhudia kuagwa kwa kundi la kwanza la asali ya Tanzania kabla ya kusafirishwa kwenda China.
“Usafirishaji wa asali hiyo unaanza kufungua fursa za masoko ya asali nje ya nchi hivyo ni Wakati sasa kwa Tanzania kujiandaa na kuchangamkia fursa za Masoko ya asali nchini China na kwingineko”. amesema Waziri Dkt. Jafo.
Dkt. Jafo pia amesema, tukio hilo si la kusafirisha asali tu bali linaashiria kutimiza maono ya ukuaji wa uchumi na ushirikiano wa kimataifa na kutoa pongezi kwa China kwa imani yao ya kuanza kusafirisha na kutumia bidhaa za asali inayotoka Tanzania.
Aidha amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi, pamoja na kuwekeza katika miundombinu ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za asali kwa wingi nchini.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments