Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni Serikali inayowajali wananchi wake ambapo inaendeleza mkakati wake wa kuhakikisha vijana wanajiajiri na kuajiriwa, kwa kuboresha na kufungua fursa kwa Wawekezaji kuja kuwekeza nchini ili kutoa ajira kwa Watanzania.
Katika kutoa vipaumbele hivyo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amesema Serikali inaendelea kushirikiana na Sekta binafsi kuboresha miundombinu ili kuongeza ajira kwa Watanzania.
Akizungumza, katika uzinduzi wa muonekano na chupa mpya ya lita moja ya juisi ya African Fruti inayozalishwa na Kampuni ya Bakhresa Food Products Limited (BFPL), Dkt. Jafo amesema Sekta binafsi inategemewa kubeba jukumu la kuongeza ajira.
“Serikali haiwezi kuwaajiri watu wote, sekta binafsi ndio nguzo ya kutengeneza ajira, na Uwekezaji kama huu unasaidia vijana na wakulima kuongeza uzalishaji,” amesema Dkt. Jafo, huku akitolea mfano wa Uwekezaji wa zaidi ya Shilingi 700 Bilioni wa Bakhresa.
Ameongeza kuwa miundombinu kama reli ya umeme (SGR) na barabara inaimarishwa ili kuchochea uzalishaji viwandani, na kuhimiza Watanzania kupenda bidhaa za ndani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Bakhresa Group, Hussein Sufian amesema, bidhaa zinazotumia malighafi za ndani huchangia kukuza uchumi na kwamba, Kiwanda hicho kimeongeza uwezo wa kuchakata matunda kutoka tani 50,000 hadi 100,000 kwa mwaka na bidhaa hizo zinauzwa katika Mataifa mbalimbali, ikiwemo Kenya, China, na Mashariki ya Kati, zikichangia fedha za kigeni na ajira kwa vijana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tetra Pak, Jonathan Kinisu, amesifu ushirikiano wa miaka 17 baina ya kampuni hizo, akisema umeleta teknolojia rafiki kwa mazingira na bidhaa bora zisizo na kemikali.
Naye Mtendaji Mkuu wa BFPL, Salim Aziz amesema, malengo ya kampuni hiyo yanaendana na ajenda ya Serikali ya kukuza uchumi kupitia bidhaa za ndani na uundaji wa ajira.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments