Wanafunzi watano wa Shule ya Sekondari Chalangwa Wilaya ya Chunya,wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa baada ya kugongwa na basi la abiria mali ya kampuni ya Safina Coach linalofanya safari kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Mbeya mjini.
Ajali hiyo imetolea leo Julai 26 mwaka huu majira ya saa 11.30 alfajiri katika kijiji cha Itumba Kata ya Chalangwa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya wakati wanafunzi hao wakikimbia mazoezi ya mchaka mchaka .
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Wilbert Siwa amewataja walio poteza maisha kuwa ni Seleman Ernest, Samweli Zambi, Kelvin Mwasamba,Hosea Mbwilo, na Amina Ulaya
Aidha ametaja majeruhi saba kati ya tisa waliolazwa katika Hosptali ya Wilaya ya Chunya na Kituo cha Afya Chalangwa kuwa ni , Bernard Mashaka (17), Lilian Raymond (16), Kennedy Masoud (14),Vicent Malema(17),Siwema Nasib (17),Alex Peter(17),Dethani Charles(15), na wengine wawili Getruda Mwakyoma (17), na Farida Mwasongole (17),wametibiwa na kuruhusiwa.
Ameasema ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Safina Coach Kenya namba za usajili T 194 DCE lililokuwa likitokea Chunya mjini kuelekea Mbeya likiendeshwa na Dereva Abdul Hassan (28),Mkazi wa jijini hapa.
Amesema chanzo cha ajali ni dereva wa gari hilo kushindwa kulimudu na kisha kuwagonga wanafunzi hao na kusababisha vifo na majeruhi.
Imeelezwa dereva wa baai hilo baada ya kusababisha ajali hiyo ametoweka na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments