SERIKALI YATOA MIL. 220 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UTALII TABORA ZOO

 

Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika jitihada za kuinua Sekta ya Utalii nchini, imetoa zaidi ya Shilingi Millioni 220, kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya Utalii ndani ya bustani ya Wanyamapori hai "Tabora ZOO"

 

Rais Dkt. Samia, amekuwa mstari wa mbele katika kuinua Sekta ya Utalii na Uwekezaji, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitatu.

 

Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka TAWA Kanda ya Magharibi Jovin Nachihangu amesema, Jengo hilo la Kitalii ndani ya bustani hiyo, litatumiwa na wananchi kupata taarifa za vivutio vya utalii vinavyopatikana katika bustani hiyo na Kanda ya Magharibi kwa ujumla (Visitors Information Centre - VIC).

 

Katika jengo hilo pia kutakuwa na vyoo vya kisasa kwa ajili ya wageni na mabanda ya Wanyamapori walao nyama (Simba, Chui, Duma).

 

“Kabla ya maboresho ya miundombinu ya Utalii, TAWA tulikuwa tunakusanya Shilingi Milioni moja kwa mwaka, lakini baada ya maboresho katika kipindi hiki cha miaka 3 TAWA inakusanya kupitia bustani hii kiasi kisichopungua Shilingi Millioni 50 kwa Mwaka na bado tunaendelea kuhakikisha kwamba mapato yanaendelea kuongezeka” amesema Jovin.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments