Serikali ya awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Saluhu Hassan, imeendelea kuwajali wananchi wake katika Sekta ya Kilimo kwa kuwasambazia ruzuku ya mbolea na mbegu bora kwa msimu wa mwaka 2024/2025, ambapo katika kipindi cha kuanzia 1 Julai, 2024 hadi kufikia 30, Novemba, 2024, jumla ya tani 253,669.342 za mbolea zenye thamani ya Shilingi 435,724,224,815 zimenunuliwa kwa utaratibu wa ruzuku na wakulima 406,966 ambapo ruzuku ya Serikali ni Shilingi 90,485,490,128.
Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, hivi karibuni Jijini Dar es Salaam, wakati akielezea mafanikio ya Sekta mbalimbali ikiwemo Bandari ya Dar es Salaam, yaliyotokana na Serikali ya awamu ya Sita katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Vilevile, katika msimu wa 2024/2025 Serikali imepanga kutoa ruzuku ya tani 52,000 za mbegu bora za mahindi kwa wakulima ambapo hadi kufikia 30
Novemba, 2024 jumla ya tani 4,000 za mbegu bora za mahindi zenye thamani ya Shilingi 3,496,721,000 ya ruzuku zimenunuliwa na wakulima
79,335.
“Hali ya upatikanaji wa mbolea na Mbegu bora ambapo makadirio ya mahitaji ya mbolea na visaidizi vyake kwa msimu wa mwaka 2024/25 ni tani 1,000,000 ambapo hali ya upatikanaji wa mbolea nchini kufikia tarehe 30 Novemba, 2024 ulikuwa ni tani 769,060 sawa na asilimia 77 ya mahitaji,” amesema Msigwa.
Kiasi hicho cha upatikanaji kilitokana na bakaa ya msimu uliopita tani 260,403, uzalishaji wa ndani tani 58,669 na zilizoingizwa kutoka nje ya nchi tani 449,988.
Msimu wa Kilimo wa 2024/2025 umeanza katika baadhi ya Mikoa inayopata mvua, kuanzia mwezi Oktoba ikiwemo Mikoa ya
Mbeya, Kagera, Kigoma, Njombe, Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora,
Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Manyara, Iringa, Rukwa, Katavi na Songwe ambapo ununuzi wa mbolea na mbegu bora unaendelea, hivyo wakulima wahakikishe wana namba ya mkulima itakayowezesha kununulia mbolea na inatumika kunununulia mbegu bora
za mahindi kwa mfumo wa ruzuku.
Kwa wakulima ambao hawajapata namba hiyo, wajitokeze kwenye ofisi za vijiji/mitaa kwa ajili ya kujiandikisha kwenye daftari la mkulima pia Wataalam wa kilimo katika ngazi za Wilaya na Vijiji/mitaa kwa kutumia vishikwambi walivyopewa, waongeze kasi ya usajili wa wakulima kwenye mfumo ili kuwezesha wakulima kupata namba zitakazotumika kununualia mbolea na mbegu bora za ruzuku.
Amesema, Halmashauri zote Tanzania Bara zitoe kipaumbele katika uimarishaji na ugharamiaji wa huduma za ugani kwa kuhakikisha kwamba, kila Afisa Ugani anatumia vitendea kazi alivyopewa na anatekeleza wajibu wake kwa kuwahudumia wakulima ipasavyo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments