SERIKALI YAHIMIZA UMAKINI UBORESHAJI DAFTARI LA MPIGA KURA

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imewataka Waandishi Wasaidizi na waendesha vifaa vya Biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya, kutambua umuhimu wa zoezi la Uboreshaji Daftari la Wapiga kura, na wanapaswa kwenda kulitekeleza kwa umakini mkubwa, zoezi linalotarajiwa kuanza Disemba 27,2024 hadi Januari 02, 2025.

 

Mwenyekiti Wa Tume Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, amezungumza wakati anatembelea mafunzo kwa Waandishi Wasaidizi wa Daktari la Kudumu la Mpiga Kura, katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma inataraji kuanza Disemba 27 mwaka huu hadi Januari 02, 2025.

 

Katika ziara hiyo, Jaji Mwambegele amekagua mafunzo kwa vitendo ya Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Biometriki (BVR) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya Disemba 24, 2024 katika Mikoa ya Mbeya, Iringa na Halmashauri ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments