Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imejipanga katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika jamii, na imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Watendaji katika Taasisi za Serikali wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi, sambamba na kuwahudumia wananchi.
Jitihada hizo za Serikali zimekuwa zikisimamiwa ipasavyo na Wakuu wa Serikali ambapo Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amekemea vitendo vya ubabaishaji na rushwa miongoni mwa Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) akisema vinaweza kufuta mazuri yote ambayo Taasisi hiyo imeyafanya na inaendelea kuyafanya.
Akiongea na Menejimenti ya TEMESA na Mameneja wa Mikoa Jijini Dodoma, Waziri Ulega ameeleza kuwa, Serikali imedhamiria kuifanya TEMESA kuwa Taasisi namba moja na kimbilio la wote katika utengenezaji wa magari ya Serikali na binafsi.
“Tunatakiwa kupiga vita sana vitendo vya ubabaishaji na rushwa, huu ndio ugonjwa unaoharibu Taasisi nyingi na kwa kweli tunahitaji kutumia uwezo wetu wote kupambana na jambo hili,” amesema Ulega.
Mkutano huo ni wa kwanza wa Waziri Ulega na Viongozi wa TEMESA tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Wizara hiyo mwezi huu.
“Hongereni kwa kuanzisha mkakati mpya wa kufanya kazi utakaowawezesha kujiendesha kibiashara kwa kushirikiana na Sekta binafsi pale inapobidi ili kuihudumia Jamii kikamilifu, sisi TEMESA lazima tuwaoneshe Watu ukinilipa nitakufanyia kazi kwa wakati,” amesema.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments