Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa wito kwa Watanzania kuendelea kulinda amani, upendo,umoja na mshikamano wetu kwa maslahi ya taifa.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa wakati alipoungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kiruruma katika Ibada ya Krismasi, Disemba 25,2024
“Tukipendana tutakuwa wamoja, tutakuwa na amani, lakini kuna tunu nyingine ya ujirani mwema na kufanya matendo ya huruma” amesema Bashungwa
Bashungwa amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kidini likiwemo Kanisa Katoliki ambalo ni miongoni mwa Makanisa yenye mchango mkubwa katika kuwakumbusha Watanzania kuishi kwa upendo na amani.
“Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikia na taasisi za dini likiwemo Kanisa letu Katoliki kwa kuwa ni miongoni mwa makanisa yanafundisha Watanzania kuwa raia wema” amesisitiza Bashungwa
Awali, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kiruruma, Padre Salapioni Mberwa amewaasa Waumini wa Kanisa Katoliki kuiadhimisha Sikukuu ya Krismasi kwa kukumbuka upendo wa Mwenyezi Mungu kwa Wanadamu.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments