SERIKALI YAWATAKA WAWEKEZAJI/WAZALISHAJI KUTHIBITISHA BIDHAA KABLA YA KUINGIA SOKONI

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imewataka Wawekezaji, wazalishaji na wafanyabiashara Mkoani Pwani, kusajili majengo yanayotumika kuuza na kuhifadhia bidhaa za Chakula na vipodozi na wale wenye viwanda wahakikishe wanathibitisha ubora bidhaa zao kabla ya kwenda sokoni.

 

Meneja Kanda ya Mashariki TBS Bi. Noor Meghji, ametoa rai hiyo kwenye Maonesho ya Viwanda na uwekezaji yaliyofanyika Mkoani humo ambapo amewataka wazalishaji wadogo nao kuthibitisha bidhaa zao, kwani Serikali ya awamu ya Sita, kupitia TBS inatoa huduma ya uthibitishaji bure hivyo kinachotakiwa ni wao kutambuliwa na SIDO .

 

"SIDO ni Taasisi mama inayohudumia wazalishaji wadogo, basi itakapo kutambulisha kwetu huduma ya uthibitishaji wa bidhaa hiyo unakuwa ni bure, kwa hiyo hakuna sababu yoyote ya kupeleka bidhaa sokoni bila kuwa na nembo ya ubora," amesema Meghji.

 

Amepongeza jitihada ambazo zimefanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ya kufanikisha maonesho hayo na kwamba TBS imeshiriki ili kuwahimiza washiriki wa maonesho hayo kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha.

 

"Iwapo haujathitibisha ubora wa bidhaa unazozalisha, haujathibitisha ubora wa mifumo basi biashara na uwekezaji huo hauwezi kuwa endelevu," amesema.

 

Ameyataja majukumu ya TBS ni kuhamasisha masuala ya viwango, kufanya uthibitishaji wa bidhaa pamoja na mifumo, kuwezesha upimaji wa bidhaa husika, kufanya ukaguzi maeneo mbalimbali yanayohusika na uuzaji na usambazaji wa bidhaa.

 

Kusimamia bidhaa zinazoingia nchini kuhakikisha ni zile zenye ubora na salama ndizo zinazoingia nchini kwa kufanya ukaguzi wa bidhaa kabla ya kuingia nchini.

 

Amesema TBS, inatoa huduma za kimaabara ambapo shirika hilo lina maabara tisa ambazo zinahusisha upimaji bidhaa mbalimbali.

 

"Lakini pia tunatoa huduma ya upimaji binafsi kwa wanaohitaji huduma hii, kwa mfano mzalishaji yeyote anayetaka kuuza nje ya nchi kuna huduma TBS tunatoa kuwezesha wazalishaji kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi.

 

"Unaweza kuwa unataka kupeleka bidhaa nje ya nchi ukaambiwa tunataka bidhaa hiyo iwe imetambuliwa na Taasisi kutoka nchi yako ambayo inathibitisha ubora na usalama wa bidhaa hiyo, basi TBS tunatoa huduma hiyo". amesema.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments