VIONGOZI CCM YASEMENI MAZURI YA SERIKALI AWAMU YA SITA

 

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt Tulia Ackson amewataka viongozi ndani ya chama  kuyasema mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita  chini Rais Samia Suluhu Hassan.

 

Dkt,Tulia ambaye  ni Spika wa Bunge na Mbunge  Mbeya mjini, amesema hayo leo Jumatatu Desemba 23,2024 ,aliposhiriki  mkutano  wa viongozi wa CCM ,uliofanyika katika ukumbi wa Dkt,Tulia uliopo sabasaba jijini hapa.

 


Amesema viongozi na wanachama wa CCM wajipe nafasi kubwa ya kuisemea serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa wananchi na  kuyatangaza mazuri yaliyofanywa katika uongozi wake.

 

"Ndugu zangu leo tumekutana hapa kueleza mambo kadhaa yaliyofanywa hususan katika Jimbo la Mbeya mjini katika sekta ya elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara njia nne,"amesema.

 

Amesema katika sekta ya elimu tumeona ujenzi wa miundombinu ya vyumba vya madarasa vya kisasa ambavyo vimeleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.

 

Dkt. Tulia amesema  uwekezaji katika miradi ya kimkakati inampasa kila kiongozi kuwa na wajibu wa kusimama na kuyazungumza  na sio kukaa kimya .

 

"Serikali imefanya na inaendelea kufanya kazi kubwa sana katika maeneo mbalimbali nchini hivyo ni wakati wenu kutumia fursa mnazopata kuyasema yaliyo kwenye maeneo yenu hususan ninyi viongozi wa serikali za mitaa,"amesema.

 

Amesema kukaa kimya kunatoa fursa kwa watu kuinuka na kuzungumza kuwa serikali haijafanya jambo lolote wakati sote tunashuhudia namna inavyosogeza huduma kwa jamii yakiwemo maeneo ya vijijini.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments