WIZARA YA MAJI YANUFAIKA NA ZIARA YA RAIS SAMIA KOREA

 

Ziara mbalimbali zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan nje ya nchi zimekuwa na tija kubwa kwa Tanzania.

 

Miongoni mwa ziara hiyo ni ile aliyoifanya nchini Korea Kusini mwaka huu, ambapo matunda ya ziara hiyo yameleta tija kwenye sekta ya maji nchini ambapo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amekiri hilo kwa kusema ziara iliyofanywa na Rais Samia nchini Korea Kusini imetengeneza mahusiano mazuri na kuchangia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya mradi mkubwa wa maji safi na usafi wa mazingira.

 

Akizungumza Disemba 16,2024 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka Katika Jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Ziara ya Waziri Aweso na timu nzima ya sekta ya Maji Nchini Korea Kusini.

 

 Waziri Aweso amesema baada ya Rais Samia kufanya ziara Korea Kusini, hatimae nae akapata nafasi ya kualikwa huko, na kwamba haijafika hata wiki nchi imepata zaidi ya dola za kimarekani milioni 240  kwa ajili ya uwekezaji kwenye maji taka.

 

Ameongeza kuwa hiyo inathibitisha mahusiano mazuri na urafiki wa thamani uliopo baina ya nchi hizi mbili  ikichangiwa na ziara ya Rais Samia nchini humo.

 

 "Si jambo jepesi kwenda na muda mfupi huo huo ukapata pesa hii ni kazi kubwa, ni kazi nzuri ya mahusiano na kujitoa kwake Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan"

 

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemshukuru Balozi wa Korea Kusini nchini Eunju Ahn kwa kuwa sehemu kubwa ya kusaidia kupatikana kwa miradi hiyo.

 

"Nipende kumshukuru sana Balozi wa Korea Mheshimwa Ahn haya mafanikio tuliyoyapata ni kutokana na ushirikiano mkubwa huwezi ukafanya kazi peke yako"

 

Mradi huo utagharimu zaidi ya dola milioni 90 sawa na bilioni 170 mpaka utakapokamilika ambapo Waziri Aweso amesema itakuwa suluhisho kubwa kwa changamoto za maji.

 

 "Kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam kutoka asilimia 45 ya sasa hadi asilimia 65."

 

Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments