'MAREKANI' YAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA KWENYE MRADI WA SGR

 

Marekani kupitia Balozi wake hapa nchini, Michael Battle ameimwagia sifa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha kikamilifu mradi wa Treni ya Kisasa ya (SGR).

 

Sifa hizo za Balozi amezitoa kupitia Ukurasa wake wa Mtandao wa "X".

 

Battle ameandika kuwa: Treni kutoka Dar hadi Dodoma. Nimepanda treni kwenye mabara manne na ninajivunia kusema kuwa Tanzania inatoa uzoefu bora wa treni. Treni iliondoka stesheni kwa wakati halisi, safari ilikuwa ya starehe na ukarimu na umahiri wa wafanyakazi ulikuwa bora."

 

Hatua hiyo ya mwakilishi wa Marekani kuipongeza Tanzania ni kubwa na ni   fahari kwa Watanzania wote.

 

Kimsingi kama nchi inapaswa kujivunia kazi nzuri inayofanywa na Serikali kwa kutekeleza miradi mingi mikubwa ya kimkakati chini ya Rais Dkt.Samia.

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments