WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA SERIKALI MBEYA WADAKWA

 



Polisi Mkoa wa Mbeya imesema limewatia nguvuni wafanyabishara wawili kwa makosa ya kuhujumu miundombinu ya Umeme na Maji.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti katika eneo la Block T na Nzovwe jijini hapa.

 

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni mfanyabiashara wa vifaa vya umeme,Joseph Movin (53) na Rehema Jamson (42) mfanyabiashara wa vyuma chakavu.

 


Kuzaga amesema watuhumiwa hao wametiwa nguvuni baada ya kufanyika msako wa kushtukiza katika maeneo  yao ya biashara na stoo za kuhifadhia vifaa.

 


Amefafanua kuwa katika msako huo Jeshi la Polisi lilishirikiana na maofisa wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) mikoa ya Nyanda za Juu Kusini  na wataalam wa Mamlaka ya Maji Mbeya.

 

Amesema msako huo ni endelevu umefanywa kufuatia kuibuka kwa watu wasio wema kuhujumu miundombinu ya Taasisi za kiserikali hususani vifaa vya Transfoma, nyaya za copper  na vifaa vya Maji 

 

️ Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments