Meneja wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya NMB Makao makuu, Sofia Mwamwitwa amesema wameanzisha kampeni ya Mastabata la Kibabe yenye lengo la kuhamasisha wananchi kutumia benk hiyo katika kupata huduma za kifedha.
Ameyasema hayo leo January 4, 2025 mjini Mtwara wakati wakiendesha droo ya kupata washindi wa kampeni hiyo, iliyofanyika AM Shoppers na kueleza kuwa kupitia droo hiyo, wametoa zawadi kwa washindi zaidi ya 30, miongoni mwao wapo walioshinda pesa tasrimu shilingi 50,000, kufanyiwa manunuzi ya shilingi 300,000, Miavuli, Tisheti, Kofia pamoja na chupa za kisasa za NMB.
Hata hivyo amesema kuwa kampeni hiyo ni endelevu ambapo ilianza mwezi wa Novemba na kilele chake kinatarajiwa kufanyika mwezi Februari 2025.
"tumefanya challenge hii katika mikoa tofauti na tukimaliza hapa tunaenda mkoa mwingine kwa washindi watakao shinda kwa mwezi wapili tutawatangaza mapema ili waweze kwenda kusherehekea msimu wa wapenda nao Dubai ambapo watalipiwa kila kitu na Benk ya Nmb.” Amesema Mwamwitwa.
Kwa upande wake Frank Tegile, ambaye ni mmoja kati ya washindi walioshinda zawadi ya kufanyiwa manunuzi ya bidhaa za shilingi 300,000 na benk hiyo amesema amefurahishwa na ushindi huo kwani hakutarajia kama angepata vitu vyenye thamani hiyo.
"kiukweli nimefurahi sana mana jumamosi kama hii narudi nyumbani na vitu hivi vingi vinavyogharimu shilingi laki tatu kwangu sio jambo la kawaida kwakuwa sikutarajia kupata". Ameeleza Frank.
✍️ Zamzam Jambia-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments