RUWASA LINDI WAPEWA WIKI 2 KUKAMILISHA VIOSKI VYA MAJI

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imetoa wiki mbili kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, (RUWASA), kukamilisha ujenzi wa miundombinu kama vioski katika visima ambavyo ujenzi wake unaendelea ili wananchi wa maeneo ambayo hawakufikiwa na miradi mikubwa waanze kupata huduma ya maji safi, salama na yenye kuwatosheleza.

 


Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva, Januari 21, 2025, wakati wa ziara maalumu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji Wilayani humo.

 

Mradi huo wa uchimbaji Visima tisa kati ya kumi Wilayani Lindi, ni miongoni mwa utekelezaji wa mikakati ya Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Watanzania katika maeneo yote nchini, wanapata huduma ya maji safi na salama.

 


Katika ziara ya kukagua Visima hivyo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mwanziva amemshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 12.79 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 13 ikiwemo miradi 5 ya uchimbaji wa visima kwa Jimbo la Mtama na Bilioni 5.71 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 17 ndani yake ya uchimbaji wa visima.

 

“Kutokana na uhitaji mkubwa wa maji, visima vinachimbwa ili wananchi warahisishiwe kupata huduma, nawaomba sana Ruwasa nitakaporudi tena nikute maji Mwamwamwa,” amesema Mwanziva.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments