Taasisi ya Tulia Trust inayojihusisha na kuwezesha wananchi kiuchumi na misaada kwa jamii imepanda miti zaidi ya 500 katika Kata tisa jijini Mbeya kwa lengo la kuhamasisha utunzaji mazingira na kurejesha uoto wa asili.
Kampeni hiyo endelevu ambayo imeanza rasmi jana Ijumaa Januari 14,2025 ikiongonzwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust , Joshua Mwakanolo.
Mwakanolo ameongoza zoezi hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye ni Spika wa Bunge, Mbunge wa Mbeya mjini na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt Tulia Ackson.
Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha jamii hususani mashuleni utunzaji mazingira kwa kupanda miti rafiki inayo himili mabadiliko ya tabia nchi.
Ametaja maeneo yaliyopandwa miti ni Kata za Iganjo, Iduda, Uyole, Igawilo, Nsalaga, Itezi, Isyesye, Ruanda na Sinde ambapo kila kata imepandwa miti 56 ya kivuli na matunda.
Amesema kampeni hiyo ni endelevu na itazifikia kata zote 36 za Jiji la Mbeya kwa kupanda miti ya matunda na vivuli na hii ni awamu ya pili huku lengo ni kupanda miti 2000.
Mkazi wa Nsalaga Seleman Juma amesema kampeni hiyo iendane na kutoa elimu kwa jamii kuelewa umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti na kutunza rasirimali hiyo.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments