Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwatia moyo na motisha wanawake maeneo mbalimbali nchini kutokana na utendaji wake uliotukuka ambapo wakati anaingia madarakani baadhi ya watu walionesha mashaka juu yake kutokana na jinsia yake.
Rais amesimamia maendeleo ya sekta mbalimbali nchini ikiwemo sekta ya madini ambapo kwa upande wa wachimbaji wadogo wa madini, amehakikisha wanapata mitaji, leseni na matumizi ya teknolojia katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuwezesha kuchimba kisasa.
Mmiliki wa Mgodi wa Kwasakwasa uliopo kijiji cha Msesule kata ya Mapogoro, wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Bi. Amagite Mkumbwike amesema, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka mazingira wezeshi ikiwemo bei nzuri sokoni ili wachimbaji wadogo waweze kunufaika zaidi.
“Nikiwa mchimbaji mdogo na mmiliki wa mgodi wa Kwasakwasa, nitaendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana na kurudisha faida kwa kile kinachopatikana katika vijiji vinavyozunguka mgodi wetu,
Serikali imerahisisha vitu vingi ikiwemo kuhakikisha bei ya dhahabu sokoni zinakuwa juu ili wachimbaji wadogo tunufaike. Tumeendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa kurudisha faida kwa jamii ikiwemo kununua vifaa vya shule kwa wanafunzi wa kijiji hiki ambao wameendelea na masomo yao ya elimu ya juu, pamoja na kununua mashine ya umwagiliaji hapa kijijini,” amesema Mkumbwike.
Naye, Msimamizi wa Mgodi huo Bw. Edward Daud ameiomba Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji ili vijana wengi wapate ajira kutokana na uwekezaji unaofanywa.
“Na sisi vijana tunapoaminiwa sehemu yoyote ile tukapewa kazi basi tuifanye kwa bidii kwa asilimia 100, tuwe waaminifu kwa waliotupa dhamana,” amesisitiza Daud.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments