SERIKALI YA RAIS SAMIA KUDHIBITI TAKA MIJINI

 

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imefanya mazungumzo na wawakilishi wa JOSPONG group of companies ya nchini Ghana, kwa lengo la kujadili namna bora ya udhibiti wa taka na usimamizi wa usafi wa mazingira mijini

 

Majadiliano hayo yamefanywa na Waziri Mohamed Mchengerwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI jijini Dodoma, Febriari 14,2025.

 

Kampuni  hiyo imeonesha nia ya kuwekeza kwenye masuala ya huduma ya uthibiti wa taka na usimamizi wa usafi wa mazingira mijini.

 

Mchengerwa amefanya kikao kazi na wawekezaji hao ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya shughuli wanazozifanya katika eneo la udhibiti wa taka na usafi wa mazingira, ili kuona kama kuna haja ya kushirikiana kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments