Naibu Waziri wa Mawasilino na Teknolijia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewataka wananchi Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuchangamkia fursa ya ujio wa kambi ya madaktari bingwa wa macho kutoka nchini Ujerumani.
Kambi hiyo itaanza kutoa huduma Juni 30 hadi Julai 5, mwaka huu katika Hosptali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya kwa udhamini wa Naibu Waziri, Mhandisi Mahundi kwa kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 21,2025 Mhandisi Mahundi amesema lengo la kuleta kambi ya madaktari bingwa wa macho ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma kwa jamii.
Amesema kupitia kambi hiyo wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma za uchunguzi sambamba na kufanyiwa upasuaji mtoto wa jicho kwa watakao bainika.
Mhandisi Mahundi ameongeza kuwa hii ni mara ya pili kudhamini kambi hiyo kutoka nchini Ujerumani kuja kutoa huduma za uchunguzi wa macho katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya.
Daktari bingwa bobezi wa macho Dkt Fariji Kilewa amesema jamii ijitokeze kupata huduma ya uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho,huku akimshukuru Naibu Waziri kwa kuleta huduma hiyo kwa wakati mwingine.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments