ASKARI POLISI WAWILI WAHUKUMIWA KUNYONGWA MTWARA

 


Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa waliokuwa askari wa jeshi la Polisi wawili kati ya Saba mkoani Mtwara, kwa kukutwa na hatia ya mauaji ya mfayabiashara wa madini Mussa Hamisi Hamisi, yaliyofanyika mwaka 2022 mkoani humo.

 


Askari waliopatikana na hatia na kupewa hukumu hiyo ni Gilbert Kalanje, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya (OC-CID), na Charles Onyango, aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi.

 

Hukumu hiyo imetolewa Juni 23, 2025 katioa Mahakama hiyo na Hamidu Mwanga Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

 


Hakimu Mwanga ameeleza kuwa ushahidi uliokuwa mbele ya mahakama uliwathibitishia hatia washtakiwa hao wawili bila kuacha shaka yoyote.

 


Askari wengine watano waliokuwa wanakabiliwa na kesi hiyo wameachiwa huru baada ya mahakama kutoridhika na ushahidi uliotolewa dhidi yao.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv


Post a Comment

0 Comments