SERIKALI YA RAIS SAMIA YAKUSANYA BIL 4.5 KUPITIA MADUHULI WILAYANI NJOMBE

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 4.5 sawa na asilimia 196 ya lengo na sehemu kubwa ya makusanyo ya Maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini, yanayotokana na mrabaha, ada ya ukaguzi, ada za leseni na vibali mbalimbali vinavyotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123, Mkoani Njombe.

 

Makusanyo hayo yamepatikana katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2023/2024, ambapo  lengo la makusanyo lililowekwa ni Shilingi Bilioni 2.3, kutokana na mrabaha, tozo na ada mbalimbali, yameendelea kupaa kutoka mwaka hadi mwaka tangu kuanzishwa kwa Ofisi ya Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini.

 

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini,  Mjiolojia Abraham Nkya 

Mkazi ya Mkoa wa Njombe amesema kuwa, ofisi hiyo imeendelea kufanya vizuri kwenye ukusanyaji wa muduhuli kutokana na mikakati waliyoiweka ikiwa ni pamoja na kuimarisha ukaguzi kwenye maeneo yote yenye uchimbaji wa madini ya makaa ya mawe, na kwamba katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 Ofisi imeweka mikakati ya kuhakikisha inaendelea kuvuka lengo lililowekwa na Serikali.

 

“Mkoa wa Njombe tuna madini mbalimbali yakiwemo ya chuma, manganizi, makaa ya mawe, madini ya ujenzi na dhahabu, na kuongeza, Madini ya makaa ya mawe ndio yanayoongoza kwa kutupa mapato makubwa mfano mwaka wa fedha uliopita wa 2023/2024  madini ya makaa ya mawe pekee yaliingiza  kiasi cha Shilingi Bilioni  4.155  na kuufanya Mkoa wa Njombe kuchangia vizuri kwenye mapato ya Serikali,” amesema Mjiolojia Nkya.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments