SERIKALI YAAGIZA MIRADI YOTE NGAZI YA MSINGI ITANGAZWE KUPITIA NeST

 

Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  Mohamed Mchengerwa imewataka Wakurugenzi  wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa Nest.

 

Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi kuhusu mfumo wa Nest kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma Februari 04, 2025.

 

Amesema "baada ya kupata mafunzo haya, nendeni mkabadilike, fuateni Sheria ya Manunuzi, onyesheni mabadiliko hayo kwenye utekelezaji wa miradi na kuanzia sasa miradi yote itangazwe kupitia mfumo wa Nest na si vinginevyo, 

 

Miradi hiyo ikishatangazwa kupitia Nest hakikisheni mnaisimamia kwa Weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha iweze kuonekana" amesisitiza Mchengerwa.

 

Aidha Mchengerwa amewataka  PPRA kuhakikisha inawajengewa uwezo watumiaji wa mfumo wa Nest katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kuomba zabuni mbalimbali.

 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments