WAKAZI WA NYATWALI WAHAMA KWA HIARI KUPISHA UPANUZI HIFADHI YA SERENGETI

 

Jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuikuza Sekta ya Utalii zimesaidia kuwafungua wananchi uelewa zaidi katika Utalii nchini.

 

Hayo yamejidhihirisha Mkoani Mara baada ya  Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kutembelea eneo la Nyatwali lililopo Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara na kukagua namna zoezi la uhamaji wa hiari kwa wakazi wa Tamau, Kariakoo, Nyatwali na Serengeti linavyoendelea.

 

Wakikagua eneo hilo,  Februari 04, 2025 baada ya kupata taarifa ya maendeleo ya zoezi la Nyatwali kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Stephano Msumi ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, CPA. Hadija Ramadhani ameshuhudia majengo mbalimbali yameshabomolewa na asilimia kubwa ya wananchi wa Nyatwali  wameshahama na zoezi la ulipaji fidia ya makaburi linaendelea kwa utaratibu mzuri na utulivu.

 

"Ninawapongeza sana kwa kuendesha zoezi hili kwa mafanikio, mmefanya zoezi kwa weledi na kwa muda mfupi. Tumeshuhudia nyumba zimeshavunjwa na zoezi la uhamishaji makaburi linaendelea  bila shaka wengine waje wajifunze kutoka kwenu zoezi kama hili linapojitokeza." 

 

Naye, Dkt. Robert Fyumagwa amesisitiza juu ya ufuatiliaji wa fedha zilizobaki ili zoezi hilo liweze kukamilika.

 

"Mmefanya kazi nzuri, tumeona ushirikiano wa Wizara, TANAPA, Wilaya hadi Mkoa sasa mjitahidi kufuatilia fedha zilizobaki ili kukamilisha zoezi hili na kama mlivyosema kwenye taarifa wanyama ni wengi wanavuka kwenda Ziwa Victoria hivyo, mjipange namna ya kupunguza wanyama kugongwa". 

 

 Akizungumza ofisini kwake, baada ya kupokea ugeni wa wajumbe wa bodi ya  wadhamini - TANAPA , Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vincent N. Anney amesema “eneo hili likishakabidhiwa kwa TANAPA ni vyema mnapotangaza vivutio vya Hifadhi ya Taifa Serengeti mtangaze na Ziwa Victoria.

 

"Ziwa Victoria litangazwe kama bidhaa inayounganisha Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi zingine za maji. Hoteli zijengwe eneo hilo ili watalii waweze kufika upande huu kwa maana wanyama watakuwa wengi na itakuwa fursa kwa wananchi wa Bunda na Mkoa wa Mara kwa ujumla.”

 

Dkt. Vincent amesisitiza kuwa, ushirikiano uendelee ili zoezi liishe salama, kwa wananchi ambao wameshalipwa fidia zao tuhakikishe wanatoka eneo hilo.

 

"Tunatarajia mpaka Februari 20, 2025 zoezi la kulipa fidia ya kuhamisha makaburi liwe limekamilika, wabaki wale wachache ambao fedha zao zitakuja ili kuepuka migongano maana ng'ombe wanachungwa sana. Sasa hatujui ni wa wananchi wanaomalizia kulipwa au laa". Amesema Dkt. Vincent 

 

Eneo la Nyatwali linalofahamika kama Ghuba ya Speke lipo Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti na lina ukubwa wa ekari 14,250.

 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments