Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendelea na jitihada zake kuhakikisha watendaji wake wanapata ujuzi wa matumizi ya mifumo mbalimbali ukiwemo mfumo wa NeSt.
Kupitia dhamira hiyo, Tamisemi wameanza kutoa Mafunzo ya Mfumo wa NeST, ambapo awamu ya kwanza imeanza Februari 04, 2025 katika Ukumbi wa Mabeyo jijini Dodoma
Aidha, Mafunzo hayo yatahudhuriwa na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Miundombinu na Maafisa Manunuzi kutoka Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao ndio walengwa wakuu.
Mgeni rasmi katika mafunzo hayo anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa, viongozi wengine ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Sospeter Mtwale sambamba na Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Bw. Denis K. Simba.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments