SERIKALI YATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA AKILI

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI chini ya Mwenyekiti wake Elibarick Kingu  imeitaka Serikali kupitia Wizara ya Afya kuimarisha huduma za afya ya akili na kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini vinawezeshwa kutoa huduma za msingi za afya ya akili.

 

Hayo yamesemwa Februari 4, 2025 na Mwenyekiti huyo wakati akiwasilisha taarifa ya Kamati mbele ya Bunge la 12 la Mkutano wa 18, kikao cha sita.

 

Kingu amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la matatizo ya afya ya akili nchini hali iliyosababisha jamii kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi na kupungua kwa uwezo wa kuzalisha mali, hivyo ameitaka Serikali kuhakikisha elimu ya afya ya akili inatolewa kwa jamii pamoja na kuongeza wataalam wa kutoa huduma za afya ya akili.

 

Ameongeza kuwa, kamati hiyo inapendekeza Serikali kurejesha kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), udhibiti wa chakula na vipodozi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwani bidhaa za chakula na vipodozi zinahusiana moja kwa moja na afya ya jamii.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

 



Post a Comment

0 Comments