Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuutangaza utalii katika Mkutano wa Utalii na Uwekezaji unaoendelea katika ukumbi wa Eros Hotel, Nehru Place, Delhi, India.
Tanzania imeshiriki mkutano huo kwa kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambacho kimetoa wasilisho kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu uwekezaji wakati wa mikutano ya biashara ya ana kwa ana (B2B) sambamba na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Msafara wa Tanzania umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mh. Nkoba Mabula. Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw. Ephraim Mafuru, Wajumbe wa Bodi pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za Serikali, ikiwemo TIC.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo ni Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments