Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mtwara imevuka lengo la makusanyo katika mwaka wa fedha 2023/2024, kwa kukusanya shilingi Bilioni 116, huku lengo mama likiwa ni kukusanya shilingi Bilioni 28.
Akizungumza katika hafla ya kilele cha maadhimisho ya siku ya mlipakodi bora kwa mwaka 2023/2024, iliyowakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali wa mkoa wa Mtwara, Meneja wa TRA Mkoa wa Mtwara Maimuna Khatibu, amesema makusanyo hayo ni sawa na asilimia 410, huku akieleza malengo ya makusanyo kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025.
“Kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mtwara tuna lengo la kukusanya shilingi Bilioni 152. Ambapo katika miezi sita ya kwanza ya mwaka inayoanzia Julai 2024 mpaka Disemba 2024, tumefanikiwa kukusanya shilingi Bilioni 201.” Amesema Maimuna.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala, akasisitiza kwa wakuu wa taasisi za umma kutekeleza kikamilifu takwa la kisheria la kukata kodi ya zuio.
“hivyo muhakikishe kila kiongozi wa taasisi ya umma anafuatilia kama kodi hizi zimekatwa na kuwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mujibu wa sheria.” Kanali Sawala.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mtwara waliotunukiwa tuzo za mlipakodi bora akiwamo Hassan Tawachi, mfanyabiashara kutoka wilaya ya Nanyumbu akaeleza maoni yake akisema “dhamira yangu niwaambie tu Watanzania wenzangu Wanananyumbu wenzangu, twende tuendelee kulipa kodi kwa hiyari kwa ajili ya maendeleo yetu”.
✍️Juma Mohamed-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments