CAG YAWAPIGA MSASA WADAU ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI MBEYA


 Wadau wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Mbeya  wamepewa mafunzo ya  kufuatilia  utekelezaji wa miradi ya maendeleo  sambamba na kutoa  mapendekezo ya Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

 

Mafunzo yameanza jana Mei 14 mpaka 20,2025 katika Mkoa wa Mbeya huku lengo ni kuifikia mikoa mitano nchini kwa makundi mbalimbali.

 

Kaimu Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG),Mkoa wa Mbeya , Athuman Seleman, amesema Mei 14, 2025 wakati akifungua mafunzo ya ukaguzi wa pamoja na usambazaji wa toleo maalumu la Mwananchi  la Ripoti za Asasi za Kiraia (NGO/CSO) kutoka mikoa mitano 

 


Seleman, alifungua mafunzo hayo ya siku saba, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichele, ambayo yatahusisha mikoa ya Mara, Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.

 

Amesema serikali imekuja na mpango wa kushirikisha wadau na mashirika yasiyo ya kiserikali, vyombo vya habari ili kuwa na uelewa wa ripoti za ukaguzi na kutoa mapendekezo.

 

"Lengo ni kuhakikisha fedha za umma na rasilimali zinatumika kwa ufanisi ili kuleta matokeo kama njia muhimu ya kutekeleza utawala bora na uwajibikaji na kujenga uelewa kwa wananchi,"amesema.

 

Amesema hatua hiyo itasaidia wananchi kujua maudhui ya ripoti ya ukaguzi wa hesabu zaa Serikali  kama nyenzo ya kudai uwajibikaji katika serikali za mitaa.

 

Aidha amewakumbusha washiriki kuhakikisha wanasimamia rasilimali za umma ili kuwezesha Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutekeleza majukumu yake kwa urahisi na kuongeza uelewa kwa wananchi.

 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Focus Mauki amesema lengo la kuwakutanisha wadau wa asasi za kiraia ni kutoa elimu ya ukaguzi wa hesabu za serikali za mitaa iliyo wasilishwa hivi karibuni.

 

Amesema ili jamii ipate uelewa limeandaliwa tolea maalumu la Mwananchi kwa lugha nyepesi ili waweze kupitia hoja zilizoibuliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.

 

Amesema kupitia mafunzo hayo watakusanya maoni na kuwasilisha kwa Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ,Charles Kichele.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments