MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AfDB

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, amefanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake Dkt. Akinumwi Adesina, kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Côte D’ivoire.

 


Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Côte D’ivoire, mwenye Makazi yake nchini Nigeria Balozi Selestine Kakele, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, ambapo pamoja na mambo mengine, walijadiliana namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Taasisi hiyo ya Fedha.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments