UGANDA YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI

 




Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepokea ujumbe kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa Uganda, ulioongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa nchi hiyo, Amos Lugoloobi. Ujumbe huu uko nchini kwa ziara ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu bora za uwekezaji, hususan katika miradi ya ujenzi wa majengo ya kisasa na yenye tija.

 

Ziara hii ni ishara ya kuimarika ushirikiano wa kikanda na nafasi ya Tanzania kama kitovu cha uwekezaji Afrika Mashariki. Kituo kilitoa maelezo ya kina kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini, fursa zilizopo hususan katika sekta ya ujenzi.

 

Pia, Kituo kilisisitiza dhamira yake ya kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji, kutoa msaada wa karibu kwa wawekezaji wote wanaohitaji taarifa, usaidizi wa kiutaratibu na mwongozo wa utekelezaji wa miradi yao nchini Tanzania.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments