SERIKALI YAWASISITIZA WARATIBU WA MAABARA KUFUATA MAADILI

 

Waratibu wa Maabara nchini wametakiwa kufuata kanuni, sheria na maadili sahihi ya taaluma zao wakati wa kutoa huduma.

 

Agizo hilo limetolewa Mei 28, 2028 na Msajili wa Maabara Binafsi kutoka Wizara ya Afya, Dominic Fwiling’afu katika Kikao cha Waratibu wa Maabara wa Dodoma na Halmashauri zake.

 

“Lengo la kikao hiki ni kuendelea kuboresha huduma za maabara nchini, kujengeana uwezo na kutoa taarifa za utekelezaji kwa kila halmashauri na kujadili changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji kazi,” amesema Fwiling’afu

 

Aidha Fwiling’afu ameongeza kuwa eneo la maabara ni eneo la heshima, hivyo ukiingia maabara unatakiwa uwe na heshima kwani ni sehemu nyeti kwa ajili ya uchunguzi na utoaji wa huduma.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments