USHIRIKIANO NA WADAU UMEPUNGUZA VIFO VYA MAMA MTOTO NCHINI

 

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Waziri wa Afya Jenista Mhagama ameelezea mafanikio ya Tanzania yanayopatikana kutokana na ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na wadau ambayo ni pamoja na kupungua kwa vifo vya kina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga. 

 

Waziri Mhagama ameeleza hayo wakati akifanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Laerdal Global Health, Tore Laerdal,  ambao ni wadau wakubwa katika sekta ya afya nchini Tanzania. 

 

"Serikali ya Tanzania imejidhatiti katika kuboresha afya na ustawi wa wanawake na wasichana pamoja na watoto ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa kulenga maeneo ya kuimarisha mifumo ya afya kama ilivyoainishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)," amesema Waziri Mhagama.

 

Aidha, Waziri Mhagama amesema Serikali ya Tanzania imeanzisha mikakati mbalimbali ya kuboresha afya za wanawake na wasichana, ikiwemo kuboresha mfumo wa fedha za afya, kuanza utekelezaji wa huduma ya afya kwa wote. 

 

"Lakini pia tumeanza uboreshaji wa mfumo wa rufaa za dharura kama vile mradi wa m-mama, kufanya tathmini na ufuatiliaji wa vifo vya kina mama na watoto, kuboresha ubora wa huduma kwa wanawake, wasichana na watoto wachanga, kuimarisha ujuzi wa wahudumu wa afya kupitia mafunzo na mazoezi ya vitendo," amesema Waziri Mhagama.

 

Katika kikao hicho wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya Taasisi hiyo na Serikali ya Tanzania ili kuboresha zaidi katika maeneo hayo.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments