BARAZA LA MICHEZO LATAMBUA JUHUDI ZA RAIS SAMIA

 


Baraza la Michezo la Taifa, limetambua na kuthamini juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika tuzo za wanamichezo waliofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa zinazoandaliwa na Baraza hilo.

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla hiyo na kupokea tuzo ya kutambua mchango wa Rais Samia katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo nchini, hafla ambayo imefanyika katika ukumbi wa Super dome Masaki jijini Dar es Salaam Juni 01, 2025.

 


Lengo la tuzo hizo ni kuwaenzi na kuwatambua Watanzania wanaoiwakilisha nchi katika michezo mbalimbali duniani na kuiletea sifa Tanzania kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

 


Akizungumza Katika hafla hiyo, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita itaendelea kuwekeza katika sekta ya michezo kwa kuwa inatambua michezo ni afya, ajira, mshikamano, maendeleo lakini pia michezo ni burudani. 

 

Aidha, Majaliwa pia amekabidhiwa tuzo ya kutambua mchango wake katika kusimamia michezo nchini.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv


Post a Comment

0 Comments