Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, yamehudhuriwa na wananchi kutoka makundi mbalimbali, wakiwemo wanawake, vijana na watoto, ambao ni miongoni mwa mabalozi muhimu wa utunzaji wa mazingira.
Maadhimisho hayo yaliyoanza Juni 1, yamehitimishwa kwa mafanikio makubwa mnamo Juni 5, 2025, yakilenga kuhamasisha ushiriki wa jamii katika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Mazingira Yetu na Tanzania Ijayo Tuwajibike Sasa: Dhibiti Matumizi ya Plastili. kauli mbiu hii inasisitiza umuhimu wa hatua za haraka na endelevu katika kulinda mazingira dhidi ya uharibifu unaotokana na shughuli za kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabiawatu ili kuzuia mabadiliķo ya tabianchi na uchafuzi wa mazingira.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, ambaye amewasisitiza Watanzania kuendeleza juhudi za kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wamehudhuria, akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, pamoja na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis.
Wengine walioshiriki ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa.
Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) yamekuwa chachu ya kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira nchini.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments