Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Fredrick Sumaye amesema Rais wa Awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua milango ya kidiplomasia ambayo imechangia ushirikiano mzuri na Mataifa mengine na kuchangia ongezeko la wawekezaji kutoka nje ambao wamewekeza katika sekta mbalimbali.
Sumaye ameeleza hayo Juni 4, 2025 alipopata nafasi ya kusalimia na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mollel Papaa Wilaya ya Babati mkoani Manyara, katika ziara ya Katibu wa NEC itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla katika mikoa ya kaskazini.
Pia amesema Rais Samia amedumisha utulivu na amani katika nchi kwa kurudisha amani kwa wafanyabiashara wa ndani ambayo imekuwa ni moja ya kivutio kwa wawekezaji wengine kutoka nje.
Aidha, amesema hapo awali wafanyabiashara walifunga biashara zao na kupoteza matumaini lakini Rais Samia amerudisha utulivu amani na matumaini kwa Watanzania na pia Watanzania walikuwa wamefungiwa milango katika nchi za nje lakini Rais Samia amefungua milango ya kidiplomasia.
“Rais Samia amefungua milango ya kidiplomasia ya nje leo wageni wamejaa, watalii na wawekezaji wana imani na Tanzania na wanakuja kwa wingi kuwekeza katika nchi yetu, Watanzania tunaombwa tushirikiane nao kama ikiwezekana, mama Samia amefanya kazi kubwa sana kurudisha ushirikiano wa Kimataifa,” amesema Sumaye.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments