RAIS SAMIA AIPONGEZA TPA KWA UTENDAJI BORA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,Juni 10,2025 ameitunuku Tuzo ya Utendaji Bora Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufuatia mafanikio makubwa ya kiutendaji katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

 

Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Magogoni jijini Dar es Salaam, ambapo TPA imetoa gawio la shilingi bilioni 181.5 kwa serikali, ongezeko kubwa kutoka bilioni 153 zilizotolewa mwaka uliopita.

 

Aidha, mamlaka hiyo imefanikiwa kupunguza gharama za uendeshaji kwa kiasi cha shilingi nusu trilioni, na kuendesha miradi mikubwa kwa kutumia fedha za ndani bila utegemezi wa moja kwa moja kutoka serikalini.

 

Serikali tayari imekusanya asilimia 53 ya makusanyo yote ya mashirika ya umma, ikiwa ni ishara ya mafanikio ya miongozo ya kiutendaji iliyowekwa na Rais Samia. Mafanikio haya ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya kuimarisha utendaji katika taasisi za umma.

 

Tukio la utoaji wa gawio pia limekuwa fursa ya kujitathmini, kupima dhamira, na kuangalia mwelekeo wa mashirika ya umma nchini. Mashirika mengi yamekuwa yakitekeleza kwa mafanikio miongozo ya R4 za Rais Samia, hususan R2 (Reforms and Rebuilding), ambayo imeleta mabadiliko chanya katika utendaji wao.

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments